Masauti ft. Nadia Mukami – Kesho Lyrics
Check out “Kesho” lyrics by Masauti featuring Nadia Mukami on Kelxfy.
Kesho Lyrics
Ninachojua Uzee upo
Usichana unakwenda
Ule urembo haupo miaka zikienda
Je utanipenda nikipata michirizi
Utanipenda kikija nacho kitambi
Nauliza utanipenda
Yangu maziwa yakilala
Uzeeni Utanipenda ama utaoa tena?
Oh My baby usiwe shaka, mi mwenzako Nakupenda
Ule urembo upo ata miaka ikienda
Kwanza ndo utanoga ukipata michirizi
Sio lazima flati tummy nitacheza na kitambi
Hivyo hivyo nitakupenda hata kifuani pakilala
Nami uzeeni utanipenda nikipata kiahara
Keshoo! I hope utanipenda my baby
Mpaka Kesho! Kufa kuzikana mi nawe baby
Mpaka kesho! Niamini ntakupenda baby
Mpaka kesho! Tuzeeke na wewe my baby
Mpaka kesho mpaka kesho mpaka keshoo
Shahidi yetu Mola
Ile siku mioyo iliposhikana
Ukanipenda nami nkakupenda
Ndo nilijuwa milele hatutoachana mi nawe
Ujana ni moshi, uko sure na mimi
Tukose udosi, je utakuwa na mimi
For better for worse, iwe better for us
Hata tukiyumba mama, tuwe pamoja
Mi bado nitakupenda, kama kipato umekosa
Kesho nitakupenda, hata mgongo ukikunja
Hivi utanipenda kama mziki ukibuma
Kweli uzeeni utanipenda nikipata kiharaa
Keshoo! I hope utanipenda my baby
Mpaka Kesho! Kufa kuzikana mi nawe baby
Mpaka kesho! Niamini ntakupenda baby
Mpaka kesho! Tuzeeke na wewe my baby
Mpaka kesho mpaka kesho mpaka keshoo