Kontawa Sikuachi lyrics ft Maua Sama
Discover Kontawa’s song “Sikuachi” with lyrics featuring Maua Sama on Kelxfy. Kontawa also known as Tawa, is one of the fastest-rising artists in Tanzania after his song “Champion” went viral in 2023.
Sikuachi lyrics
Yeah yeah…aaah aah Sama
Kabla sijaswitch life hukupindua meza
Kipindi nauza mitumba natembea na nguo kariakoo magereza
Yaani kipindi sina good life, hukuwahi kunibeza
Ulinambia nitafute sana pesa kama vile mimi ndo nimepoteza
Eh! Chumba kimoja cha kupanga
Kuna doti moja tu ya kanga
Kuna kipindi nilisanda
Mpaka nikatamani nikupeleke kudanga
Baby Maisha tuliyoishi
Tusingetoboa bila ubishi
Nilivyohustle sikufichi
Ata nikinunua ugomvi nilikuwa nadai risiti
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Wao tumetoboa, amini kwamba tumetoboa
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Wao tumetoboa, amini kwamba tumetoboa
Sikuachi mpaka milele
Mungu ametuona leo tuna mapeni
Piga kazi, we songa mbele
Mungu ametuona leo zamu yangu mi na wewe
Najua haya maisha bila mwiko hauwezi ukasonga mbele
Hata kama hupendi wali lazima utafute mchele
Waliotusema vibaya wanatuonea gere
Sisi tunafuga ng’ombe wao wanafuga nywele
Baby kipindi sina pesa
Uliposikia njaa uliziba masikio
Leo nimepata pesa nianze kukukataa
Sitaki laana kama hiyo
Ukitaja watu wasiocheat, me na we tumebakia
Haupendi pombe lakini una mguu wa bia
Ebu sema unachotaka mi ntakufanyia
Hata usipoona siku zako mi ntakutafutia
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Wao tumetoboa, amini kwamba tumetoboa
Tumetoboa, tumetoboa, tumetoboa
Wao tumetoboa, amini kwamba tumetoboa
Sikuachi mpaka milele
Mungu ametuona leo tuna mapeni
Piga kazi, we songa mbele
Mungu ametuona leo zamu yangu mi na wewe