Obby Alpha – Bora Kushukuru Lyrics
Read “Bora Kushukuru” lyrics by Tanzanian artist Obby Alpha. “Bora Kushukuru” is a Gospel song based on thanksgiving. The song is trending on TikTok.
Bora Kushukuru Lyrics
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hivi nilivyo
Maana hata
Kuna wengine hawajafika nilipo
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hiki nilichopata
Maana hata
Kuna wengine wamekosa kabisa
Tabasamu njoo,Nataka nibadiri
Wangu mtazamo niishi kitajiri
Na wewe maumivu njoo,Nataka nibadiri
Wangu msimamo niishi kijasiri
Ile habari ya kulialia
Kila siku nakataa (Nakataaa)
Na kama nilisainiwa
Mkataba nafuta aah
Ndugu tulowasaidia
Wakaficha makucha (Makucha).
Wao walipofanikiwa
Wakataka kutushusha aah!!!
Nafuta zile why me!! Why me!!
Sijapata kwanini? Kwanini?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi
Nafuta zile why mimi Why mimi!!
Sijapata kwanini? Kwanini?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hivi nilivyo
Maana hata
Kuna wengine hawajafika nilipo
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hiki nilichopata
Maana hata
Kuna wengine wamekosa kabisa
Na nilipo huenda
Kuna wengine wanapatamani
Zamani huko nilishakataliwa
Na watu wa nyumbani
Kile kidogo ninacholalamika
Lakini nimepata
Wengine huko
Wamepambana wamekosa kabisa
Kumbe ni bora kuridhika na hiki
Nilichopata ndio yangu ridhiki
Mungu ni Bora yeye hatabiriki
Amekupa hicho mi amenipa hikii
Nafuta zile why me!! Why me!!
Sijapata kwanini? Kwanini?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi
Nafuta zile why mimi Why mimi!!
Sijapata kwanini? Kwanini?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hivi nilivyo
Maana hata
Kuna wengine hawajafika nilipo
Bora hata nimshukuru Mungu
Kwa hiki nilichopata
Maana hata
Kuna wengine wamekosa kabisa