Diamond Platnumz – Zuwena lyrics
Check out Diamond Platnumz new song Zuwena Lyrics on Kelxfy. “Zuwena” is a song that tells the story of a girl named Zuwena. After the loss of her spouse, Zuwena faces life’s challenges, and Diamond Platnumz paints a picture of her ordeal.
Zuwena Lyrics
(Ayolizer)
Mhhh…Habari gani kaka naamini unanisikia
Mimi mzima wa Afya Mama Mungu anasaidia
Toka ulipotuacha Mahututi
Anazidiwa Bibi presha presha nae akatangulia
Bado twakuombea ulale salama pema
Japo moyoni nina dukuduku
Natamani kusema
Nisemeeeeee zile mali husia
Ulizotuhusia tuligawa Salama
Zuwena zote tukampatia tusiwe ndugu lawama
Ilaa! Zuena Kaka amebadilika sanaa
Yaan shem lake Bi zuuh wa leo
Sio yule wa jana
Natamani Ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuona (Zuwena)
Ooohh Ungemuona (Zuwena)
Aahh Zuwena (Zuwena)
Oohh ungemuona Zuwena (Zuwena)
Aah! Zuwena sasa kawa chotara
Sio tena cheusi Mangala
Ngozi kaichubua awe mzungu
Anavuta na Sigara Mara
Boko mwananyamala
Anachezesha tu miamala kutwa anaisugua
Kipepe rungu tena peku bila ndala
Aaah Zuwena siku hizi anabandika kope (Zuwena)
Zuwena mipasuo kama yote (Zuwena)
Ooh Zuwena lipa shika tuondoke (Zuwena)
Aah Zuwena wanamuita cha wote Oooh oooh
Juzi kabebwa na majirani hata hajitambui (Zuwena)
Yaan kalewa tafarani kautwika mbwiiiii (Zuwena)
Zuwena sio tena wa ibada na dini
Sadaka chenji asaidie
Siku hizi kageuka pedeshee wa mjini
Kutunza bendi wamsifie
Na lile gari lako urithi wa babu la kulishia Ng’ombe
Siku hizi kama kwato kwenye vilabu linabebea pombe
Mama Dede kitandani hawez hata kutembea
Zuwena ameshindwa hata kuja kumuona panadol kumletea
Natamani Ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuona (Zuwena)
Ooohh Ungemuona (Zuwena)
Aahh Zuwena (Zuwena)
Oohh ungemuona Zuwena (Zuwena)
Siku hizi kataradadi
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Anajiita JLO
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Eti mzungu mweusi
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Anatunyoosha Baba
Anadanga anakula ndizi kwa maganda