Kontawa ft. Harmonize – Binadamu Lyrics
Check out “Binadamu” lyrics by Harmonize on Kelxfy. “Binadamu” is a song that addresses every day struggles, touching the street lives of co-existing with human beings and how bitter it might get as you head towards success.
Binadamu Lyrics
Ukiuliza kiatu ndo kitakuambia
Ni mambo mangapi mi nimepitia
Siwezi rudi nyuma
Sijakariri njia, yeah
Nishakutana na mambo mengi ya dunia
Ndo maana hapa nilipo nikikuamulia
Hushindi hata ukivaa nguo za kushindia
Hamtaki kutuona mbele kwani wenzetu mnatakaje
Tulipotoka tulimwagiwa maji ya maharagwe
Mnatuombea mabaya kwani si tuliwafanyaje
Tumekosewa na vibaka mnaomba tu angali tukabe
Na kuna vitu navifanya bana hamfanyi poa
Kwa mawazo yenyu mnadhani mnanikomoa
Kila nikianzisha penzi mnapanga kulibomoa
Au mnapanga Yesu arudi anikute bado sijaoa
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
Ukidhani mnanikomoa mimi
Nyuma kuna wengi usiowajua
Usiombe wapige goti chini
Wakusomee dua
Alhamdulilahi Mungu nashukuru
Pumzi unanipa silipi ushuru
Nipate nikose siwezi kufuru
Uzuri umeniumba tembo na sio kunguru
Sina uwoga
Mi ni maji wasiponinyua watanioga
Na wakijisumbua kuniroga
Watapoteza muda kama alotahiri shoga
Binadamu bwana, eti ye ndo kakupa upofu
Na yupo hadharani anasema kuwa huyaoni
Binadamu bwana
Binadamu bwana anaweza kukupa matibabu
Na kwenye dua zake anakuombea kwa Mungu usione
Binadamu bwana yeah
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
Ukiniletea ubigi, nakuletea uparking
Usinitishie uchawi, mi mwenyewe illuminati
Binadamu wana mambo ya kiwaki
Unaweza ukang’ooka meno wakakuletea mswaki
Wa kusimama na mi, wote walikaa
Leo wanashangaa ng’ombe wa maskini amezaa
Ukinichukia mi, umechukia mtaa
Na– ferry niko party nimekaa
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
Tuoneane huruma, punguzeni hujuma
Wapo wanaotutegemea nyi mtaua
(Konde Boy call me Number one)