Nay Wa Mitego – Wapi Huko Lyrics
Read Nay Wa Mitego “Wapi Huko” lyrics on Kelxfy. In the song, Nay wa Mitego describes a “country” he had visited that intrigued him.
Wapi Huko Lyrics
Raisi! The street president
Oya niaje wanangu mlinimiss?
Nilisafiri kidogo ughaibuini
Aaah uarabuni eeh
Ah ni ughaibuni
Nipo serious ebu punguza ukatuni
Huko nilipotoka bwana ni cha kipekee
Vyakula bei juu, ila pombe ndo bei chee
Hio nchi bwana uchumi wao ni tafrani
Muda wa kazi umeme haupatikani
Soka lao limechanganywa na siasa limechoka
Mashabiki sasa ndo wajuaji kuliko kocha
Ni rahisi kupata ngono kuliko chakula
Kuna wasomi wengi hakuna ajira wanazurura
Hio nchi bana kuna watu maarufu
Mastaa kuna wa kike na wa kiume
Mastaa wa kike sura nzuri tabia ni paka shume
Asilimia tisini kazi yao wanajiuza
Mastaa wa kiume ni waongo wewe
Wabongo wakasome
Fake life mitandaoni wanaishi kifalme
Na huko ni matajiri wanaishi kifahari
Maisha yao hao halisi, wana njaa kali
Tembea uone watu wako serios
Kuna madem huko wapo very fast
Unamtongoza leo na gesi inaisha leo
Kabla hujakaa vizuri na kodi imeisha leo
Mara ooh baby mchezo mwenzio sijalipa leo
Hio nchi nimeona mengi na yote nitasema leo
Bora sisi tuna afadhali kuliko wao
Aah wee! Wapi huko?
Wananchi hawasikilizwi wanalia na Mungu wao
Aah wee! Wapi huko?
Uchawa na kubeti kwa vijana huko ndo ajira yao
Aah wee! Wapi huko?
Masingle mother kibao
Utadhani labda ndio mila zao
Hio nchi bana ina vituko vingi
Wazee wa busara ndo wanatembea na mabinti
Vijana nao wanalelewa na mashangazi
Ganda la ndizi hawataki kufanya kazi
Kuna mabinti wasomi na wanategemea uchi
Hapendwi mtu huko linapendwa pochi
Wasanii wote ni chawa wa serikali
Kasoro mmoja tu nae anapigwa vita vikali
Kila siku polisi kisa kusemea wananchi
Sikufichi hio nchi hutoboi bila ubishi
Wananchi wanalalamika naye Rais analalamika
Wote mwizi wanamjua ila wanaogopa kumshika
Hio nchi, mi naiita nchi ya utata
Elimu yao ni utata
Ukiwa na elimu kupata kazi ni utata
Aah, kupata kazi connection
Na kuipata connection ni utata
Viongozi wao matajiri utata
Ila mlo mmoja kwa wananchi ni utata
Gharama za maisha ni utata
Ila nauli zao ni zaidi ya utata
Huko dollar inauzwa ila kuipata ni utata
Tembea uone watu wako serios
Kuna madem huko wapo very fast
Unamtongoza leo na gesi inaisha leo
Kabla hujakaa vizuri na kodi imeisha leo
Mara ooh baby mchezo mwenzio sijalipa leo
Hio nchi nimeona mengi na yote nitasema leo
Bora sisi tuna afadhali kuliko wao
Aah wee! Wapi huko?
Wananchi hawasikilizwi wanalia na Mungu wao
Aah wee! Wapi huko?
Uchawa na kubeti kwa vijana huko ndo ajira yao
Aah wee! Wapi huko?
Masingle mother kibao
Utadhani labda ndio mila zao